-
9/100. Utatapeliwa na kuibiwa katika safari ya kupata hazina yako.
Habari
Karibu katika Kuendelea na uchambuzi wa kitabu the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Santiago alianza safari ya kuelekea Misri ili kufika kwenye mapiramidi ambapo hazina yake ipo. Alifika Misri na hakuwa akijua kuongea kiarabu, hivyo mawasiliano yalikuwa taabu. Alienda kwenye mgahawa na hapo akakutana na kijana ambaye aliweza kuongea lugha yake.
Alifurahi sana kukutana na kijana yule na waliongea mengi, baadaye akamwambia lengo lake la kwenda kwenye mapiramidi. Kijana yule akamuuliza una fedha, maana mapiramidi yako mbali na ni safari ya muda mrefu jangwani.
Santiago akamjibu kwamba fedha anayo, basi kijana akamwambia waongozane kuelekea eneo ambalo watapata taarifa za kuanza safari, na akamuonya kwamba eneo lile watu siyo waaminifu, hivyo ampe fedha zake akae nazo.
Santiago hakuona tatizo kwa kuwa wanaongozana, basi alimpa na kuhakikisha hamwachi muda wote wanakuwa pamoja. Walipita gulioni ambapo palikuwa na watu wengi wakifanya mauzo na manunuzi, Santiago alishangazwa na vitu ambavyo hakuwahi kuviona.
Wakati anashangaa kwa vitu hivyo aligeuka kumwangalia kijana yule na hakumw+ona tena kijana yule, na hapo ndipo aligundua kwamba ametapeliwa.Hili lilimuumiza sana, kondoo ameshauza na kwenye hazina hajafika na hata tena fedha.
Kwenye safari ya kuelekea kwenye ndoto zako, utaibiwa na kutawaliwa utakutana na watu ambao utawaamini kwa ahadi na mipango yao, lakini wataishia kukuangusha na kukuibia chochote ulichonacho.
Unapokutana na hali kama hii jua siyo mwisho wa safari yako, kama ambavyo tutaendelea kijifunza kwa hatua ambazo Santiago alichukua.
Asante Sana kwa kusoma makala hii naamini unajifunza kitu, maana dhumuni yetu hapa ni kujifunza na kufanyia kazi. Nikutakie mafanikio mema.
Makala hii imeandikwa na Kemei Maureen
Mawasiliano :
Email: Kemeimaureen32@gmail.com
0713698650
-
9/100. Lipa gharama kuanza safari ya ndoto yako.
Habari
Karibu katika mchakamchaka wa kuendeleza changamoto ya siku mia moja, ikiwa leo tupo siku ya nane. Tunaendeleza pia uchambuzi wetu wa the alchemist kilichoandikwa na mwandishi Paulo Coelho. Tujifunze na kuweka katika matendo tunapoelekea katika safari ya mafanikio.
Baada ya mazungumzo ya muda na mzee yule, Santiago alimwona ni mzee mwenye busara na hivyo kuamua kushirikisha ndoto yake kuhusu hazina ya maisha yake. Mzee alimwambia ili amfafanulie basi ni lazima amlipe kwanza.
Alimwambia ampe asilimia 10 ya kondoo wake, Santiago alikubali na mzee yule alimweleza kwamba hazina ya maisha yake ipo kwenye mapiramidi ya misri, hivyo auze kondoo wake na aanze safari ya kuelekea misri.
Santiago alizidi kuchanganyikiwa, ndiyo kitu hicho ambacho mtafsiri wa Kwanza alimweleza. Lakini hakutaka kuamini, ila safari hii alilipa gharama kujua alichokuwa anakijua tayari.
Mzee huyo alimpa nasaha nyingi sana kuhusu umuhimu wa mtu kuchagua kuishi kusudi la maisha yake. Alimweleza safari iyo itakuwa ngumu sana, lakini alimpa neno moja, pale ambapo unataka kitu kweli, dunia nzima itafanya kila namna kuhakikisha unakipata.
Kuna vitu ambavyo tunavijua kwenye maisha, lakini tunavidharau na kuchukulia kawaida, ni mpaka pale tunapolipa gharama ndiyo tunaelewa umuhimu wa kile ambacho tayari tulikuwa tunakijua.
Kitendo cha Santiago kulipa gharama na hata kuuza kondoo wake, kilimsukuma kuanza safari ya kuelekea kwenye hazina yake. Kuna vitu vinakuzuia wewe usianze safari ya kuelekea kwenye ndoto yako. Lazima uwe tayari kulipa gharama ya kupoteza vitu hivyo ili uanze safari ya kuelekea kwenye hazina yako.
DUNIA INA MWONGOZO UNAOTAKA.
Haikuwa rahisi kwa Santiago kufikia maamuzi y kuuza kondoo wake. Lakini baada ya kupata nasaha za yule mzee, alikasirika na kupata matumaini kwa wakati mmoja.
Alipata hasira Kwa nini alimjua yule mzee ambaye alimweleza ukweli kuhusu kusudi lake la maisha, lakini pia alipata matumaini kwamba safari hiyo inawezekana.
Mzee alimweleza kama atajifunza kuelewa lugha ya dunia, basi majibu ya kila kitu ataweza kuyapata. Alimkabidhi mawe mawili moja jeusi na jeupe ambaye alimwambia majina ya mawe hayo ni urim na thummim. Jiwe jeusi inaashiria NDIYO na jiwe jeupe linaashiria HAPANA.
Alimweleza anapokuwa na mashaka au kuwa njia panda na asijue kipi sahihi kufanya, basi alipaswa kuuliza swali na kisha kutoa jiwe mfukoni,likitoka jeusi ni ndiyo na jeupe ni hapana.
Tunajifunza kwamba huhitaji kujua kila kitu kabla hujaanza safari ya ndoto yako, bali unapaswa kuanza, na kadiri unavyokwenda, dunia itakuwa inakupa mwongozo unaotaka.
Usianze kufikiria mambo magumu kabla hata hujaanza, inakubidhi uanze na kisha utakapokutana na ugumu, dunia itakuonesha njia ya kuvuka ugumu huo.
Rafika yangu naamini umepata kitu kitachokusaidia katika safari yako ya mafanikio.
Limeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio na maisha na pia ni mpishi wako.Nakutakia siku njema yenye mafanikio, tukutane kesho majaaliwa.
Maureen Kemei anayekujali sana
Kemeimaureen32@gmail.com
0713698650
-
8/100. Je una uhuru wa kujitegemea wewe mwenyewe?.
Habari
Karibu katika uendelezo wa kuchambua na kujifunza kutoka kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Leo tunaangazia safari ya kijana Santiago kwa kuwaangalia kondoo wake, alipata wazo kwamba kondoo wale walikuwa wanamwamini sana kwa sababu kila siku aliwapatia chukula na maji.
Kama siku moja angegeuka kuwa katili na kuamua kuwaua wote, mmoja baada ya mwingine watakuja kushtuka baada ya wengi kuwa wamekufa. Kwa sababu washamtegemea sana kiasi kwamba hawawezi kujitegemea tena wao wenyewe.
Tunapata funzo kwamba kwenye maisha tusiweke matumaini yote kwa mtu, tuhakikishe tunakuwa na uhuru wa kujitegemea sisi wenyewe.
Ndoto. Katika safari yake, Kuna kanisa chakavu ambalo alikuwa akilala wakati wa usiku. Kila alipolala kwenye kanisa lile, Kuna ndoto ambayo ilimjia ya mtoto ambaye yupo kwenye mapiramidi ya misri, anamwambia ukija hapa utapata hazina yako.
Ndoto hii ilimsumbua sana sababu hakujua maana yake. Alimtafuta mtafsiri ndoto ambaye alimweleza kwamba anapaswa kwenda kwenye mapiramidi ya misri na huko ndipo hazina yake yalipo. Mtafsiri huyo hakumtoza fedha kwa huduma Yake, bali alimwambia anapaswa kumlipa asilimia 60 ya hazina hiyo kama atapata.
Tafsiri hiyo ilimshangaza, hakutegemea pia hakujua anawezaje kufika kwenye mapiramidi hayo, hata akifika iyo hazina itakuwa wapi? Hayo ni maswali alimwuliza mtafsiri wa ndoto, ambaye naye hakuwa anayajua.
Santiago alikata tamaa na kujiambia hatokuja kuamini tena kwenye ndoto. Mara ya kwanza tunapopata maono au ndoto yetu kubwa hatuyaelewi. Tunajiona hatuna uwezo wa kufikia na hata hatujui tutafikaje.
Lakini hatupaswi kukata tamaa kwa sababu dunia Ina njia nyingi za kutuwezesha kufikia ndoto zetu.
UONGO MKUU WA DUNIA.
Baada ya Santiago kukata tamaa na ndoto yake, aliamua kuendelea na safari yake, lakini alibadili kitabu alichokuwa nacho kwa kupata kitabu kikubwa zaidi na kuamua kupumzika kwa muda.Alikaa eneo tulivu na kuanza kusoma kitabu chake.
Pembeni yake alikaa mzee ambaye Santiago hakutaka kumsemesha, lakini mzee huyo alianza kumsemesha kwa kumweleza maudhui ya kitabu alichokuwa anakisoma. Kinaeleza jinsi watu wanavyoshindwa kuchagua kuyaishi maisha yao, alisema mzee yule. Na kinamalizia kwa kusema kila mtu anaamini kwenye uongo mkuu wa dunia.
Santiago alimuuliza mzee yule uongo huo mkuu wa dunia ni upi? Mzee alimjibu kwamba katika hatua fulani ya maisha, watu huwa wanapoteza udhibiti wa maisha yao na kudhibitiwa na hatima. Wengi wanasahau ndoto zao na kufanya kile ambacho wengine wanafanya na hapo wanapoteza kabisa maisha yao.
Somo kuu tunalojifunza ni kwamba tunapaswa kuacha mara moja kuishi uongo huu wa dunia. Kila mtu amewahi kuwa na ndoto kwenye maisha yake, lakini baadaye tunasahau ndoto hiyo kwa sababu ya kazi tunayofanya ili kuendesha maisha yetu.
Wengi wakishakuwa na majukumu wanasahau kabisa ndoto zao. Usiruhusu hili litokee kwako , kama ulisahau ndoto yako ni wakati wa kuifufua sasa.
Shukrani tele kwako wewe ambaye umetembelea blog hili na kusoma makala hizi. Naamini kabisa umetoka na kitu muhimu litakalokusaidia katika maisha yako.
Limeandikwa na
mwanafunzi wa mafanikio na maisha, pia anafanya kazi za upishi.
Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa, uwe na siku njema.
Kemeimaureen32@gmail.com
0713698650
-
7/100. Je unajua kwamba ipo njia la kuishi kusudi la maisha yako?
Nakukaribisha mwanamafanikio katika Kuendeleza usomaji wetu wa kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na Paulo Coelho.
Leo tunaona wazazi wake kijana Santiago, wakimtaka awe padri ambapo ingeleta heshima kwa familia yao. Maana walikuwa Wanaishi maisha ya chini ya ukulima, ambao kila siku kazi ilikuwa ngumu na lengo ilikuwa kupata chakula.
Santiago alipowatembelea wazaziwe, aliamua kuwaeleza kusudi la maisha yake. Kwamba hakutaka kuwa padri, bali anataka kuwa msafiri.
Babaye alimweleza kuwa wasafiri ni matajiri, kwa masikini mtu pekee wa kusafiri ni mchunga kondoo. Kwa haraka Santiago alimjibu babaye kuwa anataka kuwa mchunga kondoo. Siku iliyofuata babaye alichukua akiba aliyekuwa amemwekea kama uridhi na kumkabidhi. Akamwambia itamsaidia kununua kondoo wa kuanza naye, alimtakia kheri katika safari yake.
Somo la kujifunza kwamba ipo njia ya kuishi kusudi la maisha yetu, wengi Wamekuwa wanazika kusudi la maisha yao kwa sababu mbalimbali. Wamekuwa wanaona hawana uwezo wa kuishi kusudi hilo. Santiago hakuweza kusafiri kama tajiri, lakini aliweza kusafiri kama mchunga kondoo.
HUHITAJI VITU VINGI ILI UANZE KUISHI NDOTO ZAKO.
Santiago alinunua koti, kitabu na kundi la kondoo,alihitaji hizi hili aanze safari. Koti ilimsaidia nyakati za usiku, ambazo alilala maeneo hatari. Kitabu alikisoma mchana na usiku alikitumia kama mto wa kuweka kichwa chake. Kondoo walikuwa sababu ya safari yake. Tunajifunza kwamba hatuhitaji vitu vingi ili kuanza safari yetu.
USIISHI KAMA KONDOO .
Kwenye safari yake Santiago alijifunza kitu kimoja kuhusu kondoo. Lengo la kondoo kuu ni kupata chakula na maji, wakishapata basi wanaridhika.
Kijana aligundua kitu pekee ambacho kondoo wake walijali ni chakula na maji. Akiweza kuwapatia majani mazuri na maji, basi kondoo hao waliendelea kuwa rafiki wake.
Alitafakari maisha ya kondoo hao na kuona haikuwa na tofauti, kila siku ni kuamka, kula, kunywa na kulala. Aliona kondoo hao hawajawahi kusoma kitabu kwenye maisha yao. Na hata waliposafiri, hawakuona mazingira mapya na kuyafurahia, badala yake walifikiria chakula na maji pekee.
Wengi Wamekuwa wanaendesha maisha yao kama kondoo, kila siku wanakimbizana na kazi,kwa lengo la kupata fedha ya kuendesha maisha yao. Hawapati muda wa kuyaishi na kuyafuhia maisha yao. Hawasomi vitabu na kujifunza vitu vipya. Hawasafiri na kujifunza kwenye mazingira mapya. Kwao kila siku mpya ni kama jana kutafuta chakula na maji kama kondoo.
Jambo lakutoka nalo ni kwamba tuuishi maisha yenye maana, tujifunze na kufurahia maisha. Tutapata hayo kama tutalijua kusudi la maisha letu.
Shukran sana mwanamafanikio naamini umepata kitu katika maandishi haya. Yameandikwa na mwanafuzi wa maisha na mafanikio na anafanya kazi ya upishi. Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa.
-
6/100.Safari ya kupata hazina yako.
Karibu sana mwanamafanikio, leo tunaangazia kitabu cha the alchemist kilichoandikwa na mwandishi Paul Coelho.
Hadithi hii inaeleza harakati za kijana mchungaji aitwaye Santiago ambaye alikuwa anapata ndoto za kutafuta hazina yake kwenye mapiramidi ya Misri. Anakwenda kuomba ushauri kwa mtafsiri wa ndoto ambaye anamwambia aende kwenye mapiramidi hayo.
Ilikuwa ngumu sana, safari yenye kila aina ya vikwazo ambavyo aliweza kuvivuka na kufika kwenye mapiramidi. Hata hivyo anajifunza kwamba hazina aliyokuwa anaitafuta haipo kwenye mapiramidi, bali kule alikotoka.
MWANDISHI KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE KITABU CHAKE. Paulo aliandika kitabu the alchemist mwaka 1988 kwa lugha ya kireno nchini Brazil.
Mwandishi anasema kwenye wiki ya Kwanza kitabu kutoka, ni mtu mmoja pekee aliyenunua. Ilichukua miezi mingine sita kuuza nakala nyingine moja, tena kwa yule aliyenunua nakala ya Kwanza.
Ilichukua mwaka mmoja kitabu hakikuuzwa kabisa, kitu kilichomfanya mchapaji wa kitabu kuvunja mkataba wake, na mwandishi na kukabidhi kitabu chake akiuze mwenyewe.
Kipindi hicho mwandishi alikuwa na umri wa miaka 41 na alikuwa kwenye hali ya kukata tamaa. Lakini hakupoteza matumaini, bado aliamini kitabu chake kitawasaidia wengi kujua hazina za maisha yao.
Aliamua kukiishi kitabu hicho yeye mwenyewe, kwa kuianza safari ya kufikia hazina yake,kama ilivyo hadithi ya kitabu. Alitambua hazina yake ni uandishi, hivyo alichagua kuishi hazina hiyo na kuhakikisha anashirikisha hazina hiyo kwa watu wote.
Kwenye kitabu the alchemist aliandika kwamba, pale unapokitaka kitu kweli, ulimwengu mzima unafanya kila namna kuhakikisha unakipata. Hivyo alitaka kitabu chake kiifikie dunia na hapo alianza kutafuta wachapaji na wasambazaji wengine wa kitabu hicho.
Kilichapwa na kidogo kidogo kikaanza kusambaa kwa wengi. Kilianza kupata mafanikio makubwa, kikasambaa dunia nzima na kutafsiriwa kwa zaidi ya lugha nane. Mpaka leo bado ni kitabu ambacho wengi wanapenda na kukiri kimebadili maisha yao.
Kama mwandishi angekata tamaa miaka 30 iliyopita, leo hii dunia asingepata hazina hii muhimu sana.
SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA HAPA NI.
Haijalishi unapitia ugumu kiasi gani, usiache kuamini kwenye maono au ndoto au hazina yako.
Hiki nndicho tupaswa kukipikania na dunia ukijua kweli tukitaka, basi lazima itatumia mbinu zote kuhakikisha tumekipata.
Nikushukuru kwa muda wako wa kusoma preview haya, yameandikwa na mwanafuzi wa mafanikio wa maisha ambaye anafanya kazi ya upishi. Maureen Kemei tukutane kesho majaaliwa.
-
5/100. Mambo Kumi Ya Kujifunza Kutokana Na Maisha Ya Mwanasiasa, Mwanajeshi, Na Mwandishi Winston Churchill.
Nikukaribishe sana mwanamafanikio, tukiendelea kujifunza kutoka kitabu kanuni ya mafanikio ya Dr Amani Makirita.
Churchill alikuwa waziri mkuu Uingereza mwaka wa (1940-1945) alisaidia kushinda vita kuu ya pili ya dunia.
Tunza nguvu zako. Kutokupoteza nguvu kwenye majuto au ugomvi na kutenga muda wa kujipa raha. Churchill alitumia muda wake kufanya yaliyo muhimu, alitenga muda wa kujipa raha na kufanya hobi baada ya kazi.
Nidhamu na mapenzi. Nukuu ya Churchill: ‘Sisi wote ni minyoo viumbe wadogo ambao tunakula, tunakunywa na kufa, lakini mimi nataka kuwa minyoo unaowasha taa.’ Kitu ambacho natoka nayo hapa kuwa nakataa kuwa minyoo wa kuzaliwa, kula, kujisaidia na kufa. Nachagua kuwa minyoo wakuacha alama hapa duniani, mnyoo unaokuwa mwanga kwa wengine.
Vitabu. Kupitia kusoma vitabu Churchill aliweza kujifunza mambo mengi kuhusu dunia yaliyomsaidia kwenye uongozi na hata uandishi.
Mpangilio. “Kila siku, huwa nakaa na kutafakari kama kuna kitu cha maana nimekifanya kwenye siku yangu, siyo nilichofanya, bali kile cha tofauti na chenye manufaa” Churchill.
Ninachotoka nacho hapa ni kwamba, niwe na maandalizi kabla ya kufanya lolote. La pili, nijenge utaratibu wa kuhoji kila siku yangu na kuona kama kuna cha manufaa nimekifanya.
Utaratibu wa siku. Churchill alikuwa na ratiba yake yakuendesha kila siku yake ambayo alifuata bila kuvunja.
Hobi. “Ili mtu apate furaha, anapaswa kuwa na angalau hobi mbili au tatu na zote ziwe halisi, zinazomsukuma kufanya kitu halisi,” Churchill.
Subira. Kila nabii kuna wakati analazimishwa kwenda nyikani, kukaa kwa utulivu, atafakari n kutahajudi na kurudi akiwa mtu wa tofauti kabisa,mtu mwenye nguvu zaidi, “Churchill. Alitengwa kisiasa mwaka 1929 hadi 1939,alitumia muda huo kusoma vitabu, kujenga matofali, kuchora na kuandika vitabu. Aliporudi uongozini mwaka 1939 na kuongoza wakati wa vita ya pili ya dunia, aliweza kufanya makubwa.
Ujasiri. “Never give in. Never give in. Never, never, never in anything, great or small, large or pretty. Never give in, except to convictions of honour and good sense. Never or force,never yield to apparently overwhelming might of the enemy. Chakuondoka nacho ni kuwa hakuna kukata tamaa ata kama iwe kugumu aje, lazima nipaki kwenye laini nikipambana.
Kazi. Churchill alifanya kazi masaa 110 kwa wiki, masaa 16 kwa siku. Kitu muhimu ya kuondoka nacho ni kuwa kama sipambani, kuna mwenzangu anapambana na anaweza niondoa mara moja.
Utani. Ulimzuia asipate hasira na kutumia nafasi yake ya uongozi vibaya. Kitu nimeondoka nacho nitumie utani kupunguza ukali wa chochote ninachopitia sasa.
Tumefikia mwisho wa mambo kumi ya kujifunza kutoka maisha ya Churchill. Kupitia mambo haya nmeona kwa kweli kila kitu kinawezekana. Nitatumia hobi yangu vizuri hadi nifikie ubobezi, pia nitakuwa na maandalizi kabla ya kufanya chochote.
Asante Sana mwanamafanikio mwenzangu kwa muda wako, naamini nawe kuna kitu umeondoka nacho .
Nikutakie siku njema tukutane kesho tukiendelea kujifunza katika changamoto ya siku 100.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.
-
4/100.Naendelea kusoma kitabu kanuni ya siku ya mafanikio, leo tunaangazia utulivu kwenye siku ya mafanikio.
Dr ama kocha ameshirikisha njia Mingi ya kupata utulivu wakati wa changamoto fulani. Katika ulimwengu unaozidi kelele kutoka pande zote ni vizuri sana kujitafutia utulivu wa akili, Roho na mwili.
Unapopatwa na tatizo huwezi kukimbia hilo tatizo, hadi usuluhishe. Kama vile tunavyofanya wakati tunapatwa na tatizo tunajaribu kuondokana nazo kwa kutumia vilevi, ugomvi, mabishano au safari ili tu kuondoka kwenye tukio. Lakushangaza kwamba baada ya hayo yote tatizo hilo bado zinatufuata tu.
Kocha anasema utulivu ni ufunguo wa maisha.Anatushirikisha Njia za kupata utulivu katika maisha.
Utatu wa maisha ya binadamu zinazoshirikiana, akili lazima utulie ili ufikiri kwa usahihi, Roho inabeba hisia na imani, mwili unachukua hatua kwenye kile unachoamua na unachoamini.
AKILI
Ni injini ya maisha. Hili kuweza kupata utulivu wa akili lazima kuchukua hatua zifuatazo.
Kuwa kwenye wakati uliopo, kuweka wawazo kwenye kile unachokifanya na utaona mengi mazuri.
Dhibiti kinachoingia kwenye akili yako. Dr anashirikisha kwamba ni bora kukaa mbali na simu wakati mwingine na watu wasumbufu.
Safisha akili yako.kutenga muda wa kutafakari kila fikra iliyopo kwenye akili yako, na ujiulize je inamanufaa gani? Kama halina manufaa liondoe.
Tulia na fikiri kwa kina. Kocha anatushirikisha kwamba dunia ni Sawa na maji kwenye matope yaliyokorogeka, kama tunataka kuyaona vizuri, lazima tuyaache yatulie. Matatizo mengi tunayokutana nayo kwenye maisha ni kutokana na kuchukua hatua bila ya kufikiri kwa kina, kuona kitu kwa nje na kukimbilia kuchukua hatua. Tunapaswa kutulia na kufikiri kwa kina kabla ya kufikia maamuzi. Tuaje maji yatulie ili tuone kwa usahihi.
Andika. Dr anatuhimiza tutenge muda wa kuandika mawazo yetu, tunapoandika mawazo hayo tunafikiri vizuri na kuyaelewa vizuri.
Tengeneza ukimya. Kwenye ukimya ndipo tunasikia dunia inatuambia nini.
Tafuta hekima. Dr anatushirikisha kwamba chakula cha akili ni hekima, kama tunavyolisha mwili ndivyo tunavyopaswa kulisha akili.Tunaweza lisha akili kwa kusoma vitabu, kupitia watu waliofanikiwa, kujiuliza maswali magumu ili tutafute majibu. Anahimiza kwamba kadiri unavyojifunza ndivyo unagundua kwamba hujui. Muhimu zaidi anasisitiza kwamba siku utakapojiona unajua kila kitu ndipo unaanza kuanguka.
Jiamini, usiwe na majigambo. Kujiamini ni pale unapojua ndani Yako mna uwezo na kutumia. Kujigamba ni pale unapojisifia mbele ya wengine kwamba unaweza zaidi na wakati mwingine unadanganya katika kufanya hilo.
ROHO.
Zinabeba eneo kubwa za maisha yetu, tunakuwa na furaha au kutokuwa, tunakuwa na kiasi au kupitiliza, tunakuwa na kuridhika au tamaa, tunakuwa na utulivu au kukosa.
Kutengeneza utulivu kwenye roho zetu tunapswa kuchukua hatua zifuatazo.
Chagua mema. Kufanya kilicho sahihi mara zote. Kujijengea msingi wa maadili za kufuata na kujipima nayo.
Mtibu mtoto aliye ndani Yako. Dr anashirikisha kuitafakari maisha na kukabiliana na chochote tulichopitia huko nyuma. Kukabiliana na yaliyopita na tusiruhusu yaendelee kuwa kikwazo. Utulivu wa roho unakuja pale hatuna vinyongo vyovyote vile.
Jihathari na tamaa. Dr anashirikisha kwamba tamaa ni kitu mbaya, sababu haina mwisho. Kwenye kila tamaa inayoingia, anasema ni bora kukaa nayo kwa muda bila kuchukua hatua yoyote na utashangaa jinsi tamaa hiyo itakavyopita kama harufu mbaya.
Hivyo ndivyo tunaweza imarika kiroho kuweza kuyashinda majaribu tunayopitia kwa kuwa na subira na kutofanya chochote.
Tosheka. Dr anatuhimiza tutosheke na kile tunacho na tuyatumie kuyakamilisha maisha yetu. Tunahitaji kupika hatua zaidi kwa sababu tunaweza siyo kwa sababu Kuna kitu tumekosa.
Oga kwenye uzuri wa dunia. Dr anatushirikisha kutembea msituni kuona vyumbe vya Mungu vinavyoendelea na maisha bila wasiwasi. Kwa kufanya hivyo Tunapata utulivu wa kiroho na kupata msukumo wa kutekeleza majukumu.
Kubali nguvu iliyo kuu. Kuna nguvu kubwa inayoifanya dunia iende, lazima tuikubali.
Tengeneza mahusiano mazuri yanayohitaji muda, kazi na uvumilivu. Dr anasema mahusiano mazuri yanatutaka tuwe wema, waaminifu wenye kujali, kujitoa na kuwaamini wengine.
Ishinde hasira. Dr anatuhimiza tubadili hasira na chuki ziwe upendo na shukrani. Tusukumwe na upendo kwenye chochote tunachofanya maana upendo una nguvu kubwa.
Yote ni moja. Dr anashirikisha kwamba sisi binadamu wote ni kitu kimoja. Hatufai kuruhusu chochote kitutenganishe.
MWILI.
Dr anashirikisha kwamba kila tunachoweka kwenye miili yetu na jinsi tunavyotumia na kuhifadhi miili yetu, kunachangia sana kuwa na utulivu au kukosa.
Hatua za kuchukua ili kuwa na utulivu wa mwili.
Sema hapana.Dr anatushirikisha kwamba tunaposema ndiyo kwenye vitu visivyo muhimu, tunasema hapana kwenye muhimu.
Fanya matembezi. Dr anatuhimiza ni vizuri kufanya matembezi ili kuondokana n makwamo.
Tafuta upweke kujitenga kukaa peke yako kwa muda itakupa nafasi ya kufikiri vizuri,kusali na kutahajudi.
Kuwa mtu. Dr anasema unapaswa kuwa mtu saa zote, kwa kupata muda wa kupumzika, wa kutafakari, kujua ukomo wa uwezo na kuishi ndani ya ukomo huo.
Lala. Dr anasema usingisi ni riba, tunalipwa kwa kuwa na maisha.
Kuwa shujaa, Dr anatushirikisha hapa kwamba lengo la falsafa ni kujifunza jinsi ya kufa. Njia pekee ya kujifunza kufa ni kujifunza kuishi vizuri kila siku ya maisha yetu . Kuishi kila siku kama vile ndiyo siku ya mwisho wa uhai wetu.
Nakushukuru sana mwanamafanikio kwa kusoma makala haya, imeandikwa na Maureen Kemei mwanafunzi wa safari ya mafanikio na maisha na pia mpishi wa chakula kitamu.
Nikutakie siku njema tukutane kesho.
-
3/100. Mbinu za kuweza kutumia akili vizuri, nilichojifunza kutoka kitabu kanuni ya siku ya mafanikio.
Kitabu hiki kimeandikwa na daktari wa binadamu, kocha wa wanamafanikio, mwandishi, mjasiriamali Makirita Amani.
Nimejifunza mengi sana kutoka kitabu hiki yakiwemo,Asubuhi ya Miujiza, nisikubali Kuendelea kupoteza maisha, mambo sapa ya kufanya kila asubuhi ili niwe na siku ya ushindi, hatua za kuondoka kwenye umaskini na mengine mengi. Lakini leo nmeamua kukushirikisha Machache miongoni mwa mengi mazuri ya kujifunza na kuweka kwenye matendo.
Njia ya Kwanza kabisa kati ya tabia ya kutumia akili vizuri ni.
- Kuitenga muda ambao hauruhusu usumbufu wa aina yoyote ile, na kuweka mkazo kwenye kazi yako pekee, hakuna kingine kinachoruhusiwa hapo, akili inafanya kazi kwa uwezo mkubwa kunapokuwa na utulivu.
- Dakika 90 za kwanza kwenye kazi kitumie kufanya kitu kimoja ndiyo muhimu kuliko vingine vyote,kitu kimoja ambacho ukikamilisha basi utafanikiwa sana. Fanya hivi siku 90 na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako, muhimu zaidi ni kuanzia vipaumbele sahihi.
- Baada ya dakika 90 za kwanza, muda unaopakia fanya kazi kwa dakika 60 na pumzika kwa dakika 10. Dakika 60 unazofanya kazi unafanya kazi kweli hakuna usumbufu wala kupeleka mawazo yako pengine, zikiisha unajipa dakika kumi za mapumziko. Linajenga umakini na ustahimilivu mkubwa kazini.
- Kuwa na vitu vitano vidogo vidogo ambavyo unapanga kukamilisha kila siku. Orodhesha vitu hivyo unapoianza siku yako na hakikisha unavifanyia kazi kwenye siku yako. Kukamilisha vitu vitano kila siku ni ushindi mkubwa sana kwako.
- Tenga nafasi ya pili ya kufanya mazoezi, kwa kuwa mazoezi Yana faida kubwa Sana kwenye mwili wako. Yanaweza kuwa matembezi tu lakini yakanufaisha sana pia yanaweza kupa utulivu na kuwa mbali na teknolojia. Mazoezi ya mwili ni sehemu ya mwili kujichaji mwenyewe. Unapofanya mazoezi mwili unazalisha nguvu zaidi ambayo unaweza kutumia kufanya makubwa.
- Tenga muda wa kuchua mwili wako, zipo faida nyingi za kuuchua mwili wako, Kuondoa uchovu na kuimarisha afya. Angalau mara mbili kwa wiki tenga muda wa kuchua mwili wako. Kazi unazofanya zinaweka mwili kwenye msongo ambao ukikaa Kwa muda mrefu unatengeneza magonjwa mbalimbali. Kuuchua mwili unaondoa msongo huo, hivyo hakikisha unaupa mwili huduma huo.
- Chuo kikuu cha barabarani. Kama unatumia zaidi ya nusu saa kwenda na kurudi kwenye kazi zako kila siku. Basi unapaswa kutumia muda huo kujifunza, kwa kusikiliza vitabu inavyosomwa au kusoma wewe mwenyewe. Usikubali kupoteza muda huo kwa kusikiliza habari au kuperuzi mtandaoni.
- Tengeneza timu bora, usikazane kufanya kila kitu mwenyewe, tengeneza timu bora ya kukusaidia na yale majukumu ambayo wengine wanaweza wakafanya, wape wafanye. Wewe baki na yale muhimu pekee, ambayo wewe tu ndiye unayeweza kuyafanya.
- Ipangilie wiki yako kabla hujaianza na kila unapolimaliza ipitie na kutafakari.Hakikisha unatumia wiki iyo vizuri na kuitathmini wiki pale unapolimaliza na kuiangalia jinsi ilivyokwenda ili uweze kuboresha zaidi wiki inayofuata.
- Tenga dakika 60 za kijifunza kila siku, achana na ule mda wa kujifunza asubuhi, achana na ule mda wa kujifunza ukiwa njiani.kwenye siku yako Tenga dakika 60 za kujifunza kitu kwa kina. Unajifunza kitu kitakachokuwezesha kupika hutua zaidi kwenye maisha, kazi ata biashara yako. Litakusaidia sana kuwa wa tofauti ili kupiga hatua kubwa za mafanikio.
- Nikimalizia kocha anasisitiza kwamba akili tayari tunazo na Mbinu za kutumia vizuri ni hizi hapa, kilichobaki ni mimi na wewe kuzifanyia kazi hili ziweze kuwa na tija katika safari ya mafanikio.Nikushukuru sana wewe ambaye umetumia muda wako kusoma maandishi haya naamini zitabadilisha mtazamo wako.Tukutane kesho katika changamoto ya siku Mia. Zimeandikwa na mimi mwelekea mafanikio, mwanafunzi na mpishi, Maureen Kemei.
-
2/100 Nimejifunza LEO MAMBO MUHIMU YA KUMUOMBA MUNGU KABLA NA WAKATI AMENIINUA JUU.
- Anipee moyo wa Shukrani muda wote. Moyo wa Shukrani ni muhimu sana kwa sababu kushukuru ni ibada kama ni ibada basi nikikosa nitakuwa namnyima Mungu haki yake. Lakini, pia kuna vitu nitavikosa wakati bado napambana nishukuru Mungu. Siku nitaakapopandishwa juu nishukuru pia.
- Anipe moyo wa hekima. Hekima ya Mungu ni kitu cha msingi sana kwa hivyo niombe Mungu anizidishie hekima yake ata sasa. Hata siku nitakapo Pata hitaji langu niendelee kuomba hekima ya Mungu ili iniongoze vyema na ili isifanyike kuwa kwazo kwa watu.
- Anipe moyo wa unyenyekevu. Mfalme Nebukadreza Mungu alipomuinua alikuja kusahau kama ni Mungu aliye mpa cheo na umaarufu. Hadi ikafikia hatua alitumia vyombo vya madhabahuni. Hata Mwanawe Belshaza naye alishindwa kuwa mnyenyekevu pale Mungu alipo mpa nafasi ya kuwa Mfalme juu ya wakaldayo. Mwisho alikufa pasina kufaidi ikulu. Basi ili niepukane na anguko ya kuinuliwa natakiwa kunyenyekea. Hata sasa kama bado niko chini napaswa kunyenyekea zaidi ndipo Mungu atanipeleka kule kuliko na hadhina zake.
- Anizidishie roho ya upendo. Upendo ni muhimu sana, napaswa kuomba Mungu anipe roho ya kupenda watu nikiwa chini, nipende watu nikiwa juu. Kuwapenda watu ni ibada na amri pia, Nmejifunza kwamba kumbe nisipopenda watu nakwenda kinyume na amri ya Mungu.
- Anizidishie nguvu ya kushinda majaribu. Majaribu hayawezi kukoma, nikiwa chini yatakuwepo nikiwa juu yatakuwepo pia. Ombi langu moja tu Mungu anijalie nguvu za kushinda kila jaribu lijalo juu langu.
- Aniweke mbali na kiburi. Mfalme Nebukadreza aliangamia kwa kiburi chake baada ya kupata mamlaka kutoka kwa Mungu. Alijawa na kiburi baada kuona watu wanamtii, ana mamlaka makuu. Akasahau kuwa Mungu ndiye aliyempa mamlaka yale. Mwisho akala majani kama ngombe hivyo, niombe Mungu aniweke mbali na kiburi maana ni kubaya sana.
- Anizidishie roho ya huruma. Natakiwa kuwa na Roho ya huruma nikiwa chini na siku nitakapopandishwa niwe na iyo roho pia na rehema.
Rafiki yako.
Maureen Kemei
KEMEIMAUREEN7@GMAIL.COM
-
Habari wanamafanikio!! Katika changamoto ya siku 100, leo siku ya Kwanza Nmejifunza yafuatayo. Hatua nne za kujenga au kuvunja tabia nilizojifunza kutoka kitabu cha kanuni ya mafanikio. Kilichoandikwa na Dr, kocha Makirita Amani.
Ya Kwanza ni kichocheo, huchukua taarifa kwenye akili kuhusu tabia fulani. Ni taarifa ambazo akili inapata. Kinaweza kupitia kwa kuona, kusikia, kunusa au kuhisi.
Kubadili, sheria ya Kwanza FANYA TABIA KUWA WAZI.
Njia ya kufanya tabia iwe wazi ni
1.kuwa na ubao ambao unaandika kile ambacho unataka kufanyia kazi, unapoandika na kuona kile ulichoandika ni rahisi kufanyia kazi.
2. Kuweka Nia ya kufanya kitu kama kwa maandishi kuwa katika hali fulani nitafanya kitu fulani.
3. Kuweka tabia mpya kwenye tabia ya zamani.
4. Kuboresha mazingira na kuandaa na tabia unayotaka kujenga.
5. Kuitenga eneo maalum la kufanya tabia fulani kama kusoma au kuandika.
Kuvunja, WEKA KIFICHONI. Kama Kuna tabia unatamani kubadilisha kifiche, kama kuacha kuzurura mtandaoni bila kufanya kitu yenye tija kafiche simu.
Hatua ya pili ni TAMAA.tamaa inaleta hamasa ya kuchukua hatua fulani ili uweze kupata matokeo unayotarajia.
Sheria y pili,KUJENGA, IFANYE IVUTIE.tamaa inatokana na ubongo kupata kemikali ya dopamine ambayo Inamfanya mtu ajiskie vizuri.
Baadhi ya njia za kufanya ziwe za kuvutia ni hizi.(i) Iweke tabia unayojenga na tabia nyingine ambayo tayari unapenda kufanya. Tanguliza kufanya tabia mpya kabla ya tabia uliyozoea.
(ii) zungukwa na watu ambao nao wanafanya tabia ile unayotaka kujijengea. Sisi binadamu ni viumbe vya jamii, huwa tunaiga yale ambayo wengine wanafanya.
(iii). Chagua mtu sahihi ya mfano kwako anayefanya au alikuwa anafanya tabia iyo unayojifunza.
(iv). Ihusishe tabia unayojenga na matokeo chanya.
Kuvunja, IFANYE ISIYOVUTIA. Kubadili mtazamo juu ya tabia hiyo. Orodhesha hasara ya tabia iyo.
Hatua ya tatu. KUCHUKUA HATUA. sheria ya tatu, kujenga, IFANYE TABIA KUWA RAHISI KUFANYA. Igawe tabia kwenye hatua ndogo ndogo ambazo unazoweza kufanya bila ugumu wowote. Kadri unavyorudia ndivyo tabia inavyojengeka kwenye akili.
Yafuatayo ni mambo ya kufanya tabia kuwa rahisi.
(I). Ondoa msuguano au ukinzani, hakikisha uhitaji nguvu nyingi kufanya tabia husika.
(ii).tengeneza mazingira kuwa rahisi, kama kusikiliza audio za vitabu wakati unafanya mazoezi.
(iii) tumia sheria ya dakika mbili, jiambie kama nafanya kwa dakika mbili tu, ukishaanza ni rahisi Kuendelea.
(iv). Tengeneza mazingira ya kuvunja tabia kuwa kugumu kwako kuliko Kuendelea. Kwa mfano,kama umekuwa unajiambia utaanza biashara lakini huanzi,lipia kabisa eneo la biashara, hivyo litakusukuma kuanza. Kwa sababu usipoanza fedha zitapotea.
Kuvunja, IFANYE KUWA NGUMU. Tabia unazotaka kuzivunja, niweke ugumu katika kuzifanya.
Hatua ya nne. ZAWADI.
Lengo kuu la kuchukua hatua ni kupata zawadi. Zawadi inaturidhisha kwa kutuliza tamaa na kutufundisha kwa kuweka Kumbukumbu kwenye akili kwamba kama nataka kupata zawadi fulani basi nichukue hatua sahihi.
Sheria ya nne. IFANYE TABIA YENYE KURIDHISHA.kujenga, IFANYE YA KURIDHISHA. Iwe inakupa msukumo wa kuirudia tena kwa kufanya yafuatayo.
(I). Ifanye zawadi kuwa ya haraka, fanya matokeo kuwa ya haraka litakusukuma kufanya zaidi.
(ii). Jipe mda kila unapokamilisha kufanya tabia mpya unayotaka kujenga, kwa kupata zawadi, unasukumwa kufanya zaidi.
(iii). Kuwa na njia ya kufuatilia maendeleo yako ya kila siku, weka alama kwenye calenda, kadiri alama zinavyokua, lengo lako linakua kutovunja minyonyororo. Hivyo, utaendea ndivyo usiharibu maendeleo yako.
(iv). Tumia sheria ya kutokukosa mara mbili, unapokutana na dharura, usikose mara mbili.
5. Kuwa na mtu unayeshirikiana naye kwenye kujenga tabia, iwapo mtu uyo hatakuwepo hutataka kumwangusha bali utaendelea kufanya.
Kuvunja, IFANYE ISIYORIDHISHA. Unafanya kwa kutumia hatua mbili
Ya Kwanza, kutafuta mtu unayemheshimu, kisha kumwomba akusimamie kwenye kuvunja tabia hiyo. Unamwahidi kwamba hutafanya tabia hiyo na kuweka wazi. Hatua hizo zinapaswa ziwe zinakuumiza kiasi kwamba ukifikiria kufanya unakosa kabisa msukumo.
Ya pili, kuweka mkataba hadharani ya kuvunja tabia iyo na kuweka gharama au adabu kali pale ambapo utarudi kwenye tabia iyo.
Ndugu yangu hayo ndiyo nmekuwa nikijifunza kutoka katika kitabu cha kanuni ya mafanikio. Nmeanza kufanyia kazi na ninaona matokeo, kitu kizuri ni Kuendelea kufanya kila siku bila kukoma.
Asante Sana kwa kuchukua muda wako makini sana na kuyasoma makala haya. Anayekuleta makala haya ni mimi wako mwaminifu na mwanafunzi Maureen Kemei.