28/100.mambo sita ya kufanya kila siku asubuhi ili kuwa na siku ya ushindi.

Karibu, nikushirikishe ninayozidi kujifunza kutoka kitabu makini mno cha kanuni ya siku ya mafanikio. Iliyoandikwa na kocha Dr Makirita Amani.

Nimejifunza kwamba;

Maisha yetu yana maeneo manne muhimu tunayopaswa kuweka nguvu na umakini zetu kama tunataka kuwa na maisha bora.

Maeneo haya manne ni afya ya mwili, akili, hisia na imani.
Afya ya mwili inahusisha hali ya mwili na nguvu tulizonazo.
Akili inahusisha fikra zetu na mtazamo tulionao.
Hisia inahusisha zile hisia tunazokuwa nazo kwenye maisha.
Imani inahusisha roho na nguvu kubwa isiyoonekana ambayo inatutawala wote.

Ili tuwe na maisha yenye mafanikio tunapaswa kuyaboresha maeneo hayo manne kila siku.

Njia ya kuboresha maeneo haya manne ni kufanya mambo sita yafuatayo.

Jambo la kwanza; kukaa kimya (silence).

Hatua ya kwanza kuchukua pale unapoianza siku yako ni Kutenga muda wa kukaa kimya.

Kukaa kimya kina manufaa makubwa kwenye maisha yetu kama yafuatavyo :

1.kunaituliza akili
2.kunaiondoa msongo wa mawazo
3.kunatuwezesha kujitambua zaidi.

Baadhi ya vitu tunavyoweza kuvifanya kwenye ukimya wetu ni.

1.kufanya tahajudi
2.kusali na kuomba
3.kutafakari kwa kina
4.kupumua kwa kina
5.kushukuru.

Muda wa kufanya haya ni baada ya kuamka, dakika tano za kwanza.

Jambo la pili ni kujiambia Kauli chanya (Affirmations).

Unachagua Kauli chanya ambazo zinaonesha uwezo mkubwa na jinsi ya kuufikia kisha unajiambia Kauli hizi kwa kurudia rudia.

Jambo la tatu; kutengeneza taswira chanya (visualization).

Hapa unatengeneza taswira ya jinsi maisha yako yatakuwa baada ya kufikia kule unakotaka kwenda.

Kisha kuiweka picha hiyo kwenye akili yako na kujiona kama tayari umeshapata kile unachotaka au kufikia.

Kutengeneza taswira Kuna nguvu kama ya kujiambia Kauli chanya, akili yetu inachukulia ni kitu ambacho kimeshatokea na hivyo kutuweka kwenye mazingira ya kukamilisha hilo.

Jambo la nne; kufanya mazoezi (exercise).

Mazoezi ya asubuhi Yana nguvu kubwa zaidi, kwa sababu yananipa manufaa nitakayonufaika nayo siku nzima.

Mazoezi:
– yanaboresha afya yetu
– yanaongeza nguvu
– yanaimarisha kinga ya mwili.
– yanaifanya akili ifikiri kwa usahihi.

Yanashauriwa kutenga muda wa dakika 20 kila siku kufanya mazoezi.

Jambo la tano; ni kujisomea (reading).

Njia ya mkato, ya haraka na rahisi kubadili maisha yako ni kupitia usomaji. Unaposoma kitabu, unajifunza mambo ambayo mtu mwingine ametumia muda mwingi katika kuyaishi au kuyatafiti, lakini unatumia muda mchache kuyasoma.

Kama hujifunzi huwezi ukawa na maisha yenye mafanikio, vitabu vina hazina kubwa.

Chochote unachokisumbuka nacho kwenye maisha yako, kuna majibu yake kwenye vitabu, ni wewe kujua vitabu gani, uvisome na kisha uchukue hatua.

Ujiwekee lengo la kusoma kurasa kumi kila siku, kwa mwezi unamaliza vitabu kumi, ukifanyia kazi unayojifunza hutabaki jinsi ulivyo.

Jambo la sita;kuandika mawazo (scribing).

Akili yetu huwa linapata mawazo mengi mazuri sana na mabaya.

Ili kuondokana na hali ya kupoteza mawazo mazuri, hili uyatunze na pia kujikumbusha, lakini pia linakufundisha kupangilia vizuri mawazo yako .

Kwenye kitabu changu unaandika
– Mawazo yangu mapya ninayoyapata
– yale niliyojifunza
– mpenyo ninaoupata
– magumu ninayokutana nayo
– jinsi ninavyovivuka.

Tukutane kesho katika harakati za kujifunza zaidi kanuni hizi.

Makala hii imeandikwa na mwanafunzi wa mafanikio, ushauri nasaha na uandishi.

Maureen Kemei
Blog
Kufikirichanya.wordpress.com

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment