Rafiki mpendwa sina uhakika kama itakufaa, lakini kujifunza kuhusu namna ya kuweka bajeti ni jambo la kutilia maanani kwenye maisha.
Rafiki kwanza bajeti ni mpangilio wa kipato na matumizi kwa kipindi fulani. Kuna mitazamo potofu kuhusu bajeti kama kufikiri kuwa bajeti inabana, ni kwa matajiri, kuwa mtu unajitaji kuwa na elimu ya juu sana, kuwa na bajeti ni kuonyesha majivuno na bajeti inatengenezwa na taasisi kubwa.
Rafiki hayo ni mitazamo potofu kabisa kuhusu bajeti. Basi tuangalie mambo ya kuzingatia tunapoweka bajeti ya kila siku kwenye maisha.
Mambo hayo ni kama;
- Kukokotoa jumla ya kipato unachoingiza.
- Kokotoa jumla ya matumizi unayoyafanya, bajeti zinatakiwa kubadilika kulingana na matumizi ya mwezi husika.
- Chagua kanuni ya kugawa kipato chako.
- Gawa kipato kwenye mafungu kabla ya kutumia.
- Balance matumizi yako yasizidi kipato
- Kuwa na mpango wa kuongeza kipato.
- Bajeti ibadilike kulingana na malengo husika.
- Endelea kufuatilia bajeti ambayo umeiweka.
Chukua hatua; Rafiki tunapozingatia mambo hayo wakati wa kuweka bajeti tutaweza kufikia malengo ya kifedha na kuweka matumizi mabaya ya fedha, na kwa kufanya hivyo, tutaweza kufikia uhuru wa kifedha.
Rafiki yako,
Maureen Kemei.