Rafiki yangu mpendwa karibu leo tujitamkie kauli kumi chanya ya mafanikio ambazo zinaelekeza fikra kwenye malengo, zinapunguza mawazo hasi,zinaongeza motisha ya kuchukua hatua, zinaimarisha imani binafsi, na pia zinajenga nidhamu ya muda mrefu.
Hizi ni kauli 10 chanya tunazoweza kujitamkia kila siku.
- Nina uwezo wa kujenga biashara yenye mafanikio na thamani kwa watu wengi.
- Kila siku nachukua hatua zinazonikaribisha kwenye uhuru wa kifedha.
- Nidhamu, uvumilivu na kujifunza kila mara vinanipeleka kwenye mafanikio makubwa.
- Ninaona fursa ambazo wengine hawazioni na nazitumia kwa hekima.
- Pesa ni matokeo ya thamani ninayotoa kwa wengine, na ninaongeza thamani kila siku.
- Biashara yangu inakua kwa utaratibu na mifumo inayoifanya ijiendeshe kwa ufanisi.
- Nina uwezo wa kufanya maamuzi sahihi yanayojenga utajiri wa muda mrefu.
- Changamoto ni nafasi ya kujifunza, kuboresha na kukua zaidi.
- Ninavutia watu, washirika na wateja wanaochangia ukuaji wa biashara yangu.
- Ninaelekea kwenye uhuru wa kifedha, amani ya akili na maisha yenye kusudi kila siku.
Hatua ya kuchukua, kaulia chanya ni kama ramani ya akili, lakini safari yenyewe inahitaji hatua za kuchukua.
Tunahitaji kuchukua hatua kama tunataka kufikia uhuru wa kifedha kama kuongeza kipato, kuwekeza,kupunguza matumizi, kujenga biashara yenye mfumo, na kuwa na nidhamu ya muda mrefu.
Rafiki yako,
Maureen .