Rafiki, najua pia wewe una hamu ya kujua njia za kufanya ili usikate tamaa kwenye safari hii ya mafanikio.
Basi usiwe na wasiwasi wowote kwa sababu niko hapa kwa ajili yako rafiki yangu, karibu tujifunze njia hizo ili kamwe tusikate tamaa kwenye maisha.
Habari njema ni kuwa watu wengi ambao wamefanikiwa kwenye maisha yao wamekuwa wakitumia njia hizi ili wasikate tamaa kwenye safari ya mafanikio.
Njia hizo ni kama yafuatayo:
- Kubali mapema kwamba safari itakuwa ngumu. Hakuna mafanikio bila changamoto.
- Weka mfumo, siyo hisia. Weka ratiba, weka malengo ya kila siku, weka viwango vya kazi . Fanya kazi hata kama hujiskii kufanya. Kocha Dr Makirita Amani huwa anasema usikubali mtu yeyote akushinde kwenye kujifunza au kusoma na kufanya kazi.
- Jifunze kutafsiri kushindwa kama somo. Rafiki badala ya kusema ‘nimeshindwa’ tunapaswa kusema “nimejifunza nini”.
- Punguza kutegemea matokeo ya haraka. Rafiki mafanikio ya kweli huchukua muda.
- Jikumbushe sababu yako [your why]. Kila unapochoka, jikumbushe kwa nini ulianza. Unapaswa kujitamkia kuwa “nataka maisha makubwa, na sitakata tamaa mpaka nipate.
Hatua ya kuchukua; rafiki pata picha unapoyazingatia mambo hayo vizuri kwa sababu zinafanya kazi vizuri sana. Utafikia ndoto zako kubwa na utaweza kufanya makubwa na kuacha alama kwenye maisha yako.
Rafiki yako,
Maureen.