Rafiki, karibu leo tunajifunza jinsi ya kuishi maisha ya furaha licha ya kukabiliana na magumu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Kwa mujibu wa wanafalsafa njia ya kupata maisha mazuri si kwa kulazimisha matokeo, bali kwa kujenga tabia na kufanya yaliyo ndani ya uwezo wako.
Mambo ya kuzingatia ili kuishi maisha mazuri ni kama yafuatayo:
- Tenganisha unachoweza kudhibiti na usichoweza kudhibiti. Unaweza kudhibiti juhudi zako, maamuzi yako na mtazamo wako. Huwezi kudhibiti maoni ya watu, bahati, au matokeo yote.
- Fanya wajibu wako kila siku. Mafanikio makubwa hujengwa kwa hatua ndogo zinazorudiwa kila siku.
- Kubali changamoto kama sehemu ya ukuaji. Kikwazo kinaweza kuwa fursa ya kujifunza na kuwa imara zaidi.
- Tawala tamaa na hisia zako. Usifanye maamuzi muhimu ukiwa na hasira, woga, , au msisimko mkubwa.
- Thamini kile ulicho nacho sasa. Shukrani huleta utulivu na hukusaidia kuona fursa zilizopo.
Hatua ya kuchukua; Lenga kuwa mtu bora kila siku; matokeo mazuri yatafuata.
Rafiki yako,
Maureen.