Rafiki karibu kwenye siku ya leo tunajifunza jinsi ya kuepuka utegemezi mkubwa kutoka familia na watu wa karibu.
Familia haihitaji mafanikio ya mmoja kama nyenzo ya kufanya bidii maishani bali ni utegemezi mkubwa ambao huchosha kiakili na watu hutoa huku wakiwa na maumivu ndani yao.
Baadhi ya mambo ya kufanya ili kuondokana na utegemezi huu ni kama yafuatayo;
- Jitoe kwenye janga la umaskini . Maisha ya watu huendelea hata nafasi ya wewe kusaidia watu ikipotea.
- Weka bajeti ya kusaidia watu. Mfano; fungu la mwezi la kusaidia watu labda ni 100,000. Budget ikiisha na shughuli imekwisha pia. Mpango wako ni muhimu kuliko chochote kile.
- Sio muda wote tatizo hutatuliwa kwa pesa. Mfano; mpe kazi mpe ushauri, mpe connection.
- Fundisha watu kujitegemea. Weka masharti ya pesa yako kwa maana pesa si rahisi.
- Jifunze kusema ‘hapana’ hakuna kusema ngoja tuangalie, unampa mtu matumain8 na usumbufu unakuwa mwingi.
- Tengeneza mfuko wa familia.
- Epuka maonyesho ya maisha yanakufanya uonekane una fedha nyingi.
- Badilisha falsafa ya familia.
Hatua ya kuchukua; Rafiki tunapaswa kujenga familia sio za kutegemea bali kushirikiana kwa lengo la kuvunja umaskini na kujenga utajiri wa vizazi.
Rafiki yako,
Maureen.