Mambo 4 yakuzingatia ili kuwa na nidhamu kali ya kuamua na kutenda

Rafiki yangu mpendwa karibu sana kwenye blog hii ya kujifunza kila siku. Nimerudi sasa tusonge mbele na kujifunza kila siku, naamini uko salama sana.

Leo tunajifunza kuhusu nidhamu ya kuamua kufanya, tunapopanga kufanya kitu lazima tupange na kufanya. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwenye maisha kwa sababu ya kukosa nidhamu hii.

Watu wengi hukosa nidhamu kwa sababu hawajaamua kwa dhati, hawana mifumo ya kuwasaidia na hawana watu wa kuwawajibisha.

Mara nyingi mtu huanza jambo kwa hamasa kubwa, lakini hatua ya kuendelea kulifanya kila siku bila sifa wala makofi ndiyo sehemu ngumu na yenye mafanikio ya kweli.

Mambo ya kuzingatia ili kuwa na nidhamu ni kama ifuatavyo;

  1. Badilisha utambulisho wako. Jione kama kile unachokitaka kuwa. Ukiwa mfanyabiashara tenda kama mfanyabishara, ukiwa mwandishi,andika kila siku.
  2. Tengeneza mifumo. Usitumie nguvu binafsi pekee kwa sababu unaweza kuchoka au kurudi nyuma ukipata changamoto. Mfumo mzuri hukusaidia kuendelea hata ukiwa huna hamasa.
  3. Tengeneza mazingira yanayokuunga mkono. Mazingira yana nguvu kubwa katika kufanikisha au kuharibu malengo yako.
  4. Kuwa na uwajibikaji. Pata mtu wa kukusimamia au coach wa kukuwajibisha ili usijidanganye na kuacha ulichoamua kufanya.
  5. Jamii ya watu wanaokuzunguka. Huwezinirudishia kufanikiwa katika jambo kubwa kama bado una tabia au watu wanaokurudisha nyuma.

Mifano ya tabia zinazoweza kukukwamisha ni kama: visingizio, uvivu, kukosa uaminifu, uzinzi, uongo nk.

Rafiki ukiwa karibu na watu wenye tabia hizo, ni rahisi kurudi kwenye mazoea mabaya na kushindwa kusonga mbele kadri muda unavyokwenda.

Hatua ya kuchukua; rafiki washindi au wanaofanikiwa hufanikisha mambo yao kwa nidhamu kali ya kuamua na kufanya na si kwa bahati. Naamua leo kuwa naweka kali katika kazi na shughuli zangu za kila siku.

Rafiki yako,

Maureen.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment