Njia 2 Za Kuongeza Kujikubali Wewe Mwenyewe.

Karibu rafiki nini tunachoweza kufanya na maisha yetu yanatokana na historia na mtazamo wa maisha yetu.

Unakuta mtu anafanya makubwa na anapata matokeo lakini hajikubali. Kama anaweza kufanya zaidi ya hapo, anaanza kuogopa na kujidharau kupitia ujumbe hasi ambao umekuwa unaupokea mara kwa mara siku za nyuma.

Njia ya kutoka kwenye hali ya kutokujiamini, kutokujithamini na kutokujikubali ni kwa kujiambia maneno chanya mara kwa mara bila kuacha.

Kitu cha pili ni kusanya ushahidi wa zile kauli chanya unazojiambia kupitia matokeo unayopata hata kama ni machache na endelea kupiga hatua.

Hata kama matokeo yamekuja tofauti na ulivyotegemea, badala ya kuhalalisha kwamba mimi siwezi kufanya vizuri na watu wengine wanathibitisha hilo kukudhibitishia kuwa huwezi, unapaswa kujiambia kauli chanya ya kuboresha makosa kama vile wakati mwingine nitafanya hivi na vile.

Chukua hatua; rafiki tunapaswa kufanya tuwezavyo kwa chochote tunachofanya na malengo yetu. Kwa kujithamini,kujiamini na kujikubali.

Rafiki kwa kila hatua unayotaka na kufanya jiambie kauli chanya.

Mwandishi wako,

Maureen Kemei .

kemeimaureen7@gmail.com.

uamshobinafsi.com.

By Maureen Kemei

Author, psychologist.

Leave a comment