Matatizo makuu mawili kwenye zama tunazoishi.

Karibu rafiki, Kuna matatizo makubwa mawili yanayokumba watu wengi kwenye zama hizi. Tatizo la kwanza ni kuishi kwa mazoea na kufuata mkumbo. Yaani kufanya kile ambacho wengine wanafanya na wamezoea kufanya na kusahau upekee ambao upo ndani yao. Tatizo la pili ni watu kutokujali kile wanachokifanya, kiwe ni kazi au biashara watu wanafanya tu kwa… Continue reading Matatizo makuu mawili kwenye zama tunazoishi.

Kutoogopa kukosea.

Kila mtu ameumbwa akiwa na uwezo wa kujaribu kufanya vitu vipya. Hivyo, tunapojaribu kufanya vitu hivyo vipya makosa hayana budi kutokea. Kwa hivyo hatupaswi kuogopa kukosea maana ni njia moja ya kujifunza na kujiboresha zaidi. Anayeogopa kufanya makosa hataki kukuwa au hataki mabadiliko yoyote katika maisha yake. Ndio maana ni muhimu kutumia nguvu iliyo ndani… Continue reading Kutoogopa kukosea.

Kutengeneza mtazamo sahihi.

Mtazamo ulionao yana mchango kubwa Sana kwenye matokeo unayopata kwenye maisha yako. Upo hapo ulipo sasa kutokana na mtazamo ambao umejijengea siku za nyuma. Na mtazamo ulionao leo, ndio utakaokujengea kesho yako. Watu wengi wana mtazamo hasi na ambao unawazuia kufanikiwa hata kama wamejiwekea malengo makubwa na wanajua kusudi la maisha yao. Mtazamo wa wengi… Continue reading Kutengeneza mtazamo sahihi.

Kupata mrejesho wa kweli kutoka kwa watu sahihi.

Unahitaji watu ambao wamebobea kwenye kile unachofanya na ambao wapo tayari kukupa mrejesho wa kweli hata kama utakuumiza. Wawe tayari kukuambia ni wapi unakosea au wapi una udhaifu. Watu hawa wanaweza kuwa waalimu, makocha mashauri na mamenta. Huwezi kubobea kama hupati mrejesho wa kweli kutoka kwa wale wanaoelewa kile unachofanya. Ni rahisi kujidanganya mwenyewe kwamba… Continue reading Kupata mrejesho wa kweli kutoka kwa watu sahihi.

Aina za mtazamo.

Kuna aina mbili za mtazamo, mtazamo mgando na mtazamo wa ukuaji. Kila mtu ana mtazamo hii miwili ndani yake, kwenye baadhi ya mambo mtu ana mtazamo mgando na mambo mengine mtu ana mtazamo wa ukuaji. Mtazamo wa mgando sanasana unaleta fikra zinazoweza kukukwamisha. Ilhali mtazamo wa ukuaji unaleta fikra chanya zinazokusaidia upige hatua zaidi. Unapaswa… Continue reading Aina za mtazamo.

Unachohofia mara nyingi huwa hakipo.

Mara nyingi kile tunachohofia hata huwa hakitokei. Ni sisi tu binadamu huwa tunatengeneza mazingira ya hofu ambazo hata kiuhalisia hazipo. Hofu huwa tunatengeneza akilini. Baada ya kuijaza hofu akilini mwili unapokea matokeo yake na hapo tunashindwa kuthubutu na kufanya kile tulichochagua kufanya. Dawa ya hofu ni kukabiliana nalo mzima mzima, bila kujali nini kitatokea hata… Continue reading Unachohofia mara nyingi huwa hakipo.

Kupata tumaini la maisha.

Zawadi tuliyopewa sisi wanadamu siyo kuona bali kuwa na maono makubwa juu ya maisha tunayotamani kuyaishi. Lakini, ni muhimu pia kufurahia kile ulicho nacho wakati unapambana kupata kilicho kubwa zaidi. Hapo ndipo chanzo cha tumaini kinaanza, kufurahia ulichonacho huku ukiwa makini usiridhike sana na hapo ulipo. Unapambana kufikia ndoto na maono yako makubwa. Hiyo ni… Continue reading Kupata tumaini la maisha.

Unatumiaje muda wako?

Karibu, nikushirikishe ninayojifunza kutoka kitabu cha Pata masaa mawili ya ziada kila siku. Kilichoandikwa na kocha Makirita Amani. Japokuwa wote tuna masaa 24 kwa siku, matumizi yetu hayafanani. Wapo wanaotumia vizuri muda wao na wanaofanikiwa na wale wanaoshindwa wanatumia vibaya. Chochote unachofanya kwenye maisha yako ili kuongeza kipato, Kuna muda ambao unatumia kwenye shughuli hiyo… Continue reading Unatumiaje muda wako?

Zawadi ambayo tumepewa kwa usawa.

Rafiki, karibu nikushirikishe yale ninayojifunza kutoka kitabu pendwa kiitwacho Pata masaa mawili ya ziada kila siku. Kilichoandikwa na Kocha Makirita Amani. Mwandishi anaanza kwa kusema tumepewa zawadi ya muda kwa usawa kabisa, ni sisi wenyewe tunachagua tuitumieje zawadi hii ya kipekee. Mwandishi anaendelea kusema hakuna anayeweza kukunyima muda au kununua ya ziada hata kama ana… Continue reading Zawadi ambayo tumepewa kwa usawa.

Kutafuta thamani yako.

Unapaswa ujue kuwa uwezo wako upo wapi alafu utapeleka nguvu zako pale ambapo uwezo wako upo. Itambue thamani yako baada ya kujua usiache thamani yako ipotee bila kutumika au kwa lugha rahisi usitumie thamani chini ya viwango. Binadamu ana bahati sana maana ana uwezo mkubwa ulioko ndani yake. Hakuna kitu ambacho binadamu hawezi ni ile… Continue reading Kutafuta thamani yako.